Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 5, 2013

CHAMA CHA WAENDESHA BAJAJI MKOA WA MBEYA CHATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA UYOLE MBEYA

Chama cha waendesha bajaji na walezi wao wakikabidhi msaada wa chakula kwa mlezi wa kituo cha Nuru kilichopo Uyole jijini Mbeya
Chama cha waendesha bajaji wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao yatima wa kituo cha Nuru
Mlezi wa madereva wa bajaji Mwaka Mwakisu amewasisitizia madereva bajaji kuwa kile kifaida kidogo wanachopata katika kazi yao ni muhimu kuwakumbuka watoto yatima kwani ni jukumu letu kuwalea watoto hawa maana ni wetu sote pia vijana tuache ngono uzembe alisema Mwakisu
Mlezi watoto hao katika kituo hicho, Rose Kawiche, akiwashukuru chama hicho cha madereva wa bajaji kwa moyo wao huo wa kuwajali watoto hao na amewaomba wasichoke kuwatembelea mara kwa mara watoto hao kujua wanaendeleaje
Mwenyekiti wa waendesha bajaji mkoa wa Mbeya Iddi Ramadhani amewataka vijana wenzie kuacha tabia ya kuwapa mimba mabinti na kicha kuwaacha matokeo yake hao mabinti nao hutupa hao watoto yaani huwezi amini hapa huwenda mmoja wetu anamtoto hapa hivyo basi jamani tuwatunze hawa watoto na kuwasaidia mara kwa mara maana huyu mama mlezi peke yake hawezi alisema Iddi
Katibu wa bajaji mkoa wa Mbeya  Ernest Mwaisango amesema chama chao sasa kimejipanga vizuri kuwasaidia watoto yatima na wanaje mkoa wa mbeya kwani kipato chao kidogo kitatosha kugawana na yatima hao
Mlezi wa chama cha madereva wa bajaji Aneth au mama Somji amewataka wanawake waache kutupa watoto maana sasa tunawapa watu wengine shida ya kuwalea
Wanachama wa bajajiwakiondoka mara baad ya kutoa msaada wa chakula kituoni hapo




  Chama Cha Waendesha Bajaji Jijini Mbeya, kupitia kwa mlezi wao, Mwaka Mwakisu wametembelea  kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Kilichopo Uyole ambapo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo ni vyakula vyenye thamani  ya shilingi 320,000.

Mlezi wa chama hicho cha waendesha Bajaji, Mwaka Mwakisu, alitumia fursa hiyo  kuwataka vijana na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa huruma na kutojihusisha na matukio ya unyama kama hayo ya kutupa watoto wasiokuwa na hatia.

 “Kama tulivyosikiwa wenyewe vijana hapa historia ya watoto hawa kutoka kwa mlezi wao, alivyosema kuwa tangu kuanzishwa kwake kwa kituo hiki walianza na watoto wawili mwaka 2013 lakini leo hii wamefikia idadi ya watoto 17 na kibaya zaidi mama huyu anasema watoto wamekuwa wakiokotwa wakiwa wametupwa majalalani na kutelekezwa”  

“Jamani hali hii inatia uchungu kwa kweli watoto kama hawa  hali waliyonayo ni lazima ifike mahala jamii hususani akina dada kuwa na moyo wa huruma  kuliko kuwa na moyo wa kikatili kama huu” alisema Mwakisu.

Aidha, Mwakisu aliwataka vijana na jamii kwa ujumla kuwa walinzi wa karibu kwa akina mama ambao wanaona wapo katika hali ya ujauzito kuwachunga na kwamba pindi atakapoonekana kutokuwa na ujauzito ni bora akaulizwa  na kama hana mtoto achukuliwe hatua zaidi ili kuweza kupunguza idadi ya watoto yatima.

 Awali Mlezi watoto hao katika kituo hicho, Rose Kawiche, alisema kuwa ongezeko la watoto wanaotupwa limekuwa likiongeza siku hadi siku.

“Kwa kweli idadi ya watoto imekuwa ikongzekeza siku hadi siku kwa mfano kwa mwaka jana pekee tumepokea watoto watano na sasa ninawatoto 17, na hawa wote ni wale wamekuwa wakiokotwa majalalani wakiwa bado kichanga na kwamba kama hawa mnaowaona hapa umri wao hauzidi miezi sita na saba” mpaka  miaka mitano alisema mama huyo huku akionekana kutokwa na machozi.

1 comment:

Anonymous said...

Ni wakati wa watanzania wote kutumia nafasi zetu ktk kusaidia watoto yatima kama walivyofanya hiki chama cha bajaj kwanza nawapongeza sana kwa moyo huo na mungu awabariki sana.