Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, April 14, 2013

WANANCHI Wilayani Rungwe wameaswa kutunza vyanzo vya maji pamoja na mazingira ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa asasi zisizokuwa za kiserikali zinazohamasisha suala la maji.

Afisa wa Maji wa bonde la Ziwa Nyasa, Wilgal  Mkondola, aliyesimama wakati wa warsha iliyowajumuisha wenyeviti wa vijiji vyote vya halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe,
Mtendaji Mkuu wa Elimisha, Festo Sikagonamo, alisema kuwa lengo la kuwashirikisha wenyeviti wa vijiji vyote vya Halmashauri hiyo ya Busokelo, ni kutaka kuwakutanisha na wataalum mbalimbali wa mazingira ili kujadili  na kuweza kuangalia namna ya kutunza  na kuhifadhi vyanzo hivyo vya maji na sambamba na kuangalia vyanzo vya kuharibika kwa vyanzo vingine vilivyopo kwenye maeneo husika.

WANANCHI Wilayani Rungwe wameaswa kutunza vyanzo vya maji pamoja na mazingira ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa asasi zisizokuwa za kiserikali zinazohamasisha suala la maji.

Mamlaka ya maji ya bonde la Ziwa Nyasa, imesema kuwa itaenedelea kushirikiana na asasi zisizokuwa za Kiserikali, kuhakikisha  inatoa elimu kwa wananchi  na wadau wa maji ilikutambua umuhimu wa kutunza vyanzo vyote vya maji vinavyotililisha katika ziwa hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa wa Maji wa bonde hilo la Ziwa Nyasa, Wilgal  Mkondola, wakati wa warsha iliyowajumuisha wenyeviti wa vijiji vyote vya halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe, iliyoandaliwa na asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Elimisha ya Jijini Mbeya huku ikiwa na lengo la kujadili na kutambua vyanzo vyote vya maji vilivyopo ndani ya halmashauri hiyo na chgangamoto zake.

Alisema kuwa ili kukabiliana na janga la kupungua kwa maji katika vyanzo mbalimbali vya maji Serikali inatambua umuhimu wa kushirikiana na  asasi za kiraia kwa kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa vyanzo hivyo.

Alisema kuwa kilio kikubwa  duniani kote ni kupungua kwa maji baridi kutokana  na uharibifu  wa mazingira ambao kwa nman moja ama nyingine unatokana na shughili za kibinadamu hivyo Serikali kwa kushirikiana na asasi za kiraia zainawajibu wa kuelimisha wananchi ili kujiokoa na janga linaloonekana kujitokeza.

“Nia ya Serikali ni  kushirikiana na asasi zisizokuwa za  kiraia  ili kufikia malengo yanayokusudiwa kwa jamii nzima, na hivi sasa  duniani kote kuna kilio kikubwa cha uharibifu wa mazingira wa kupungua na kutoweka kwa maji  katika vyanzo hivyo ndio maana asasi hii imeliona suala hili la utunzaji vyanzo vyetu vya maji na kuandaa warsha hii,’’alisema Mkondola.

Mtendaji Mkuu wa Elimisha, Festo Sikagonamo, alisema kuwa lengo la kuwashirikisha wenyeviti wa vijiji vyote vya Halmashauri hiyo ya Busokelo, ni kutaka kuwakutanisha na wataalum mbalimbali wa mazingira ili kujadili  na kuweza kuangalia namna ya kutunza  na kuhifadhi vyanzo hivyo vya maji na sambamba na kuangalia vyanzo vya kuharibika kwa vyanzo vingine vilivyopo kwenye maeneo husika.

“Lengo la kuandaa warsha hii ni kutaka kuwakutanisha wenyeviti wa Vijiji pamoja na wataalam wa maji kutoka bonde la Ziwa Nyasa  ili kujadili vyanzo vyote vya maji vilivyopo ndani ya halmashauri ya Busokelo na kuangalia namna ya kuendelea kuhifadhi pia kuangalia sababu za kuharibika kwa baadhi ya vyanzo hivyo sambamba ili jamii ipewe elimu ya kuvijenga na kuvitunza vyanzo hivyo,” alisema Sikagonamo.

No comments: