Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, April 7, 2013

WASANII MBEYA WAZINDUKA WAANZISHA SHIRIKISHO LA WACHEZA FILAMU MKOA WA MBEYA

MWENYEKITI WA MUDA WA SHIRIKISHO LA WAIGIZAJI MKOA WA MBEYA SAMWEL MWAMBOMA AKIZUNGUMZA AZMA YA KUWAKUTANISHA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA KATIKA KIWANJA CHA CITY PUB MBEYA
KATIBU WA MUDA WA SHIRIKISHO LA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA SADY MWANG'ONDA AKIZUNGUMZIA MIKAKATI YA WASANII KUJIKWAMUA KATIKA KAZI ZAO ZA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA
BAADHI YA WASANII WA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA WAKIWA KATIKA MKUTANO ULIOWAKUTANISHA WAIGIZAJI KATIKA UWANJA WA CITY PUB JIJINI MBEYA
BAADHI YA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA WAKIWA WAMESIMAMA DAKIKA MOJA KWA AJILI YA KUMKUMBUKA MSANII MWENZAO STEVEN KANUMBA ANAYETIMIZA MWAKA MMOJA TANGU AFARIKI DUNIA APRIL 7 MWAKA JANA
BAADHI YA WASANII WALIPATA MUDA WA KUWAULIZA MASWALI VIONGOZI WAO WA MUDA NA KUCHANGIA MADA MBALI MBALI KATIKA MKUTANO HUO
MEZA KUU IKIWA MAKINI KUWASIKILIZA WASANII WENZAO WAKICHANGIA MADA
BAADHI YA VIONGO ZI WA WAKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI



WASANII wa Filamu Mkoani Mbeya wameaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kuaminiana ili kuifanya kazi zao kujulikana kitaifa na kupata masoko mengi ikiwa ni pamoja na kujiongezea kipato.

Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Filamu Mkoa wa Mbeya, Samwel Mwamboma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha kusambazia Filamu cha Sam Video Centre cha Jijini Mbeya

Mwamboma alisema Mkoa wa Mbeya unawasanii wengi sana na wazuri tofauti na Dar Es Salaam lakini wameshindwa kujulikana kutokana na kukosa ushirikiano na uaminifu unaosababishwa na ubinafsi ndiyo unaosababisha kutofanikiwa  wala kujulikana kwa wasanii licha ya kushiriki katika Filamu nyingi.

“ Wasanii mkiwaamini watayarishaji wa Filamu, Wasambazaji, Waongozaji, Wapiga Picha na Waandaaji kazi zetu zitafika mbali sana lakini mkiwa wabinafsi hatutaendelea kabisa” Aliosema Mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa Lengo la Kuanzisha Shirikisho la wacheza Filamu Mkoa wa Mbeya ni kuleta Umoja ili kazi za Wasanii wa Mkoa wa Mbeya zijulikane na kupendwa na watazamaji ili Wasanii wakubwa kutoka Dar Es Salaamu watamani kufanya kazi nao na siyo Wasanii wa Mbeya kutamani kuigiza na Wasanii wakubwa.

Kwa Upande Katibu wa Muda wa Shirikisho hilo Sadi Mwang’onda alisema kuwa moja ya vitu vinavyosababisha kazi za wasanii wa Mkoa wa Mbeya kuonekana kutokuwa na ubora ni kutokana na kila mtu kufanya kazi kivyake bila ushirikiano ambapo Watayarishaji, Wasambazaji, Wapiga picha na wadau kutokuwa na umoja.

Aliongeza kuwa Wasanii wa Mkoa wa Mbeya wanakutana na Changamoto nyingi ambazo ni ukosefu wa Mitaji  hivyo kuwaomba Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wenye mitaji kuwekeza katika Soko la Filamu ambapo aliongeza kuwa kama wasanii wako tayari kuhakikisha Mwekezaji ananufaika na hajutii kuwekeza kwenye Filamu za Wasanii wa Mkoa wa Mbeya.

Aliitaja Changamoto Nyingine kuwa ni kukosekana kwa Elimu miongoni mwa Wasanii ambapo wengi wao wamekosa elimu ya kawaida ya darasani ili  hali wengine kutokuwa na ufahamu juu ya kitu wanachokifanyia maigizo, kutokana na hilo Katibu huyo amewakikishia Wasanii kuwa baada ya Shirikisho hilo kutulia atawatafutia Semina na Mafunzo ili wapate mwanga kuhusu Filamu.

Katibu huyo alizitaja changamoto zingine kuwa ni pamoja na Wasanii kutofanya utafiti kuhusu kile anachotaka kukiigiza jambo ambalo linasababisha kazi nyingi kuonekana kama zinafanana,ukosefu wa matangazo na wasanii wenyewe kutojiamini kutokana na kazi wanazozifanya hivyo kuonekana ni wababaishaji tu.

Mbali na hayo Mwang’onda aliwasihi Wasanii waliojitokeza katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Wasanii zaidi ya 50 kutoka Ndani ya Jiji la Mbeya, Wadau wa Filamu pamoja na Wanahabari kuwa Wasanii wanatakiwa kuishi maisha ya Heshima kama wanavyoigiza kutokana na Jamii kuiamini sana kazi za sanaa.

Aidha Katibu huyo alisema ili Shirikisho lao liweze kuimarika na kuendelea watakuwa wakifanya mikutano ya mara kwa mara na kuwataka Wasanii hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kukutana kila wanapopata nafasi na sio kubaguana.

No comments: