Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 27, 2013

AFISA Elimu Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda amewaagiza Wakuu wa Shule za Sekondari, Waratibu Elimu Kata na Maafisa Michezo kuhakikisha hawajumuishi wanafunzi wa kidato cha nne katika kushiriki mashindano ya Umiseta.

AFISA Elimu Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda amewaagiza Wakuu wa Shule za Sekondari, Waratibu Elimu Kata na Maafisa Michezo  kuhakikisha hawajumuishi wanafunzi wa kidato cha nne katika kushiriki mashindano ya Umiseta.

Afisa michezo mkoani hapa George Mbijima akitangaza matokea ya mashindano hayo






AFISA Elimu Mkoa wa Mbeya, Juma Kaponda amewaagiza Wakuu wa Shule za Sekondari, Waratibu Elimu Kata na Maafisa Michezo  kuhakikisha hawajumuishi wanafunzi wa kidato cha nne katika kushiriki mashindano ya Umiseta.


Alisema mashindano yatakayofanyika Mwakani yasiwahusishe wanafunzi wa kidato cha Nne kutokana na kuwa ni darasa la mitihani ya Taifa hivyo kuwafanya kukosa maandalizi ya kutosha pindi wanapokuwa wamechaguliwa kushiriki michezo hiyo ambayo hufanyika katika kituo kimoja ambacho ni mbali na shule zao.


Maagizo hayo aliyatoa mwishoni mwa wiki wakati akifunga Mashindano ya Umiseta kwa ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Iyunga Jijini Mbeya, mashindano yaliyohusisha wachezaji kutoka Kombaini ya timu za Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya.

Kaponda alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda hadi Taifa huwanyima fursa ya kusoma wale ambao watabahatika kufuzu ngazi zote hizo hadi mashindano ya Taifa.

Kutokana na hali hiyo zaidi ya Wachezaji 40 wa michuano hiyo waliochaguliwa kuunda timu ya Mkoa ni wanafunzi wa Kidato cha Nne ambapo walitakiwa kukaa kambini kwa ajili ya kujiaandaa na mashindano katika ngazi ya Kanda yatakayofanyika Hivi karibuni Mkoani Mbeya.

Aidha katika kilele hicho timu ya Kombaini ya Jiji la Mbeya ilifanikiwa kuchukua Kombe  la Mpira wa Miguu baada ya kufanikiwa kutinga Fainali kwa kucheza na Timu ya Kombaini ya Wilaya ya Mbozi na kushinda kwa jumla ya magoli 3 kwa moja.

Katika michuano hiyo timu hizo zilicheza kwa kukamiana ambapo katika dakika ya 14 ya Mchezo huo Jiji ilifanikiwa kupata goli la kuongoza lililofungwa na Christopher Edson, ambapo timu ya Mbozi ilisawazisha goli hilo dakika ya 22 kipindi hicho hicho na kufanya timu kwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana 1-1.
  
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Christopher Mwaipopo aliifungia timu ya Jiji goli la pili kwa Mkwaju wa Penati kufuatia kufanyiwa madhambi na mabeki wa timu ya Mbozi na Mwamuzi kuamuru Mkwaju upigwe uliozaa goli katika dakika ya 72.
  
Dakika ya 90  Mbeya Jiji  ilifanikiwa kupata goli la tatu na la ushindi kutoka kwa mchezaji wake Ipyana Muyavilwa kwa mkwaju wa Penati pia kutokana na kuangushwa katika eneo la hatari wakati mabeki wa timu ya Mbozi wakijaribu kuokoa.

  
Zaidi ya michezo sita ilishindaniwa na kutolewa makombe kwa washindi, zawadi ambazo zilizotolewa kwa ufadhili wa kampuni ya vinywaji ya Pepsi kwa michezo ya Mpira wa Miguu kwa Wanaume na Wanawake, Mpira wa Pete, Basketi Wanaume na wanawake, Voleyball wanaume na wanawake, Handball Wanaume na Wanawake pamoja na mpira wa meza na riadha.


Aidha Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda baada ya kumaliza kukabidhi makombe kwa washindi pia aliwaambia washindi kuwa makombe waliopewa ni vyao moja kwa moja hayatashindaniwa tena bali Mwakani yataandaliwa mengine.

Picha na Mbeya yetu

No comments: