Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, July 12, 2013

KAMPUNI YA HIGHLAND SEED GROWERS LTD YALETA NEEMA KWA WAKULIMA WA MAHINDI VIJIJINI.

Wakala Mkuu wa  Usambazaji wa mbegu za Highland Seed Growers, Tito Tweve.
 
 Wakala wa Usambazaji wa mbegu za Highland Seed Growers, Award Mpandile akizungumza jambo na wakulima wa Mahindi kuhusu uzuri wa mbegu hizo vijijini.
                                       
 Meneja Masoko wa Kampuni ya kuzalisha  mbegu ya Highland Seed Growers John Mbele akitoa elimu kwa Wakulima wa kata ya Ikuwo jinsi mbegu hizo zinavyostahimili hali ya hewa na mahitaji ya watanzania.
 Wakulima wa Kata ya Ikuwo wakifuatilia kwa makini elimu juu ya Mbegu ya Mahindi iliyofanyiwa utafiti na Chuo cha Kilimo cha Uyole aina ya UH 615.
 Diwani wa Viti Maalum kata ya Ikuwo Tuli Mwasanga akigawa mbegu kwa Wakulima
 Mkulima akitoa maoni yake kuhusu mbegu hizo

 Afisa Masoko akiwa katika picha ya pamoja aada ya kumaliza mkutano
 Wakulima wakigawiwa mbegu kwa ajili ya majaribio
Meneja Mauzo na Wakala  wa mbegu wakiangalia shamba la mfano lilivyozalisha vizuri


 Afisa kilimo wa kata ya Ikuwo Olimpa Ukwama  akizungumza jambo
 Diwani wa Kata hiyo Antony Sanga
 Baadhi ya Maafisa Kilimo wakitoa somo


Wakulima wakisikiliza kwa Makini .

Picha na Mbeya Yetu


********

 
Katika kuhakikisha Sera ya Serikali ya Kilimo kwanza inafanikiwa kwa Vitendo, Kampuni ya Kusambaza Mbegu Mbali mbali zinazofanyiwa utafiti na Chuo cha Kilimo cha Uyole Jijini Mbeya imeanza kuwasambazia Wakulima wa Vijijini mbegu bora za Mahindi aina ya UH 615.
 
Neema hiyo imeanza kuwanufaisha Wakulima wa Wilaya za Makete Mkoani Njombe, Rungwe na Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya baada ya Kampuni hiyo kusambaza mbegu ambazo wakulima wamezisifu kuwa zinazalisha mazao mengi tofauti na mbegu zingine.
 
Akizungumza na Wakulima wa Kijiji cha Ikuwo Wilayani Makete katika Mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya  kujua jinsi wakulima wanavyokumbana na changamoto za Mbegu hizo mpya Wakala wa Usambazaji wa Mbegu za Highland Growers Ltd, Award Mpandile amesema lengo la kutengenezewa mbegu hizo ni kukabiliana na hali halisi ya hali ya Hewa ya asili ya Mtanzania.
 
Amesema Mbegu nyingi zinazolimwa na Wakulima haziwasaidii kutokana na kutoa Pumba nyingi badala ya Unga pamoja na kushindwa kustahimili magonjwa mbali mbali hali inayopelekea Wananchi wengi kushindwa kupata maendeleo.
 
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,  John Mbele amesema ni kampuni chache zinazotengeneza bidhaa na kuwauzia watumiaji lakini baadaye wakaenda kuwauliza wananchi namna wanavyoipokea na matunda yake pamoja na changamoto.
 
Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Ikuwo wamesema mbegu zilizoletwa na Kampuni hiyo ni bora kutokana na uzalishaji wake kukidhi haja na kuwaongezea kipato.
 
Wamesema unapovuna Mahindi machache lakini unga unakuwa mwingi tofauti na kiwango hali kadhalika ladha ya unga wake pamoja na mahindi yenyewe ambayo mara nyingi huishia kuchoma na kuwaomba wasambazaji kuwaisha Mbegu hizo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwatafutia soko la uhakika kutokana na kujikita katika uzalishaji.
 
Aidha wakulima hao zaidi ya 30 walizawadiwa kila mmoja Kilo mbili za mbegu za mahindi kwa ajili ya mfano ili wapande na kujionea manufaa na ubora wa mbegu hizo kabla ya kuanza kuuziwa ili wabadilishe mfumo kutoka kutumia mbegu za zamani na kutumia mbegu za kisasa zilizofanyiwa utafiti.

No comments: