Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 14, 2013

HOT NEWS! MZEE WA MIAKA 50 MBARONI KWA KUBAKA WATOTO WAWILI UMRI MIAKA 4 NA 5 KWA KUWAPAKA MAFUTA YA KULA SEHEMU NYETI KATIKA DUKA LAKE.

MBAKAJI ERASTO MWAKYOMO (50) ANAYETUHUMIWA KWA UBAKAJI AKIWA KATIKA OFISI YA MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE KABLA YA KUCHUKULIWA NA MWENYEKITI WA DAWATI LA WATOTO NA UKATILI WA KIJINSIA MARY GUMBO.
WATOTO WALIOKUWA WAKIBAKWA WAKITOA MAELEZO JINSI WALIVYOKUWA WAKITENDEWA
 MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE CHRISTOPHER MWAKIBETE AKIANDIKA BARUA KWA WAZAZI NA MTUHUMIWA KUPELEKWA POLISI 
 BAADHI YA WAZAZI NA NDUGU WA WATOTO WAKIWA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA MTAA.


***************

Ezekiel Kamanga

ERASTO MWAKYOMA mwenye umri wa miaka hamsini mkazi wa mtaa wa Mapelele Kata ya ILEMI jijini Mbeya anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwadhalilisha watoto wawili wa kike wote wakazi wa Mapelele.

Wazazi wa watoto hao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watoto hao ambao mmoja ana umri wa miaka minne na mwingine mitano walitoa taarifa kwa Balozi wa mtaa Bwana CASIAN MWEZIMPYA ambapo baada ya kutafakari kwa kina aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Mwenyekiti wa mtaa Bwana CHRISTOPHER MWAKIBETE Aliamua kuwaita wazazi na mtuhumiwa kuwahoji yaliyotukia ambapo nao watoto walipewa nafasi ya kueleza ambao walieza kuwa ERASTO Alikuwa akiwashika sehemu za siri na kuwapaka mafuta kabla ya kufanya nao mapenzi.

Baada ya kusikiliza kwa makini MWAKIBETE aliamuru kuwa suala hilo ni la kisheria na kitaalamu hivyo hawezi kuchukua hatua zozote bali suala hilo analazimika kulipeleka Polisi ambapo Mwenyekiti wa Dawati la watoto na jinsia MARY GUMBO Alimchukua mtuhumiwa hadi kituo cha Polisi kati.

Baada ya mahojiano ya awali GUMBO aliwachuchukua watoto hadi Hospitali ya Rufaa kwa uchunguzi na mtuhumiwa kubaki kituo cha kati kwa mahojiano zaidi,hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya watoto mtaani hapo wamekuwa wakitendewa vitendo vya ukatili lakini vimekuwa vikifumbiwa macho na baadhi ya wazazi wakihisi ni aibu kwa watoto wao.

 Na Mbeya yetu Blog

3 comments:

Unknown said...

Endapo uchunguzi utaonyesha kwamba ametenda kosa hilo,afungwe asitoke kabisa!

Unknown said...

Kama uchunguzi utabani mtuhimiwa katenda kosa hilo.afungwe asitoke kabisa

Anonymous said...

Je, mtu huyu ana mke na je, ana watoto? Kwangu mm anastahili adhabu kali huko tunako elekea mbona sipati picha itakuaje? Na hao wazazi wanao waonea haya watuhumiwa na watoto wanaofanyiwa ukatili wajifunze katika hili vinginevyo watiwe mbaroni wao naona wana lao jambo!